Rais Xi Jinping wa China, ameridhia ombi la Rais John Magufuli la nchi hiyo kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari 20 wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa madaktari hao watasomea shahada ya uzamili na uzamivu katika matibabu ya Ini kwenye Chuo Kikuu cha Shandong nchini humo.

Katika taarifa hiyo imeelezwa kuwa balozi wa China nchini, Wang Ke amewasilisha ujumbe huo kwa Rais Magufuli sambamba na kutoa nafasi 30 za wataalam watakaohudhuria semina ya mafunzo ya usimamizi wa hospitali.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli alitoa ombi hilo Novemba mwaka jana wakati meli ya matibabu kutoka China ilipowasili nchini kwa ajili ya kuwafanyia vipimo na kutoa tiba kwa watu waliokuwa na magonjwa mbalimbali.

Hata hivyo, Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini. Paul Cartier baada ya Mabalozi hao kumaliza muda wao.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 7, 2018
Kwanini uajiri wahitimu wapya?