Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi ametishia kuwafuta kazi Mawaziri wake na kulivunja bunge, iwapo washirika wake wa Kisiasa ambao wanaegemea katika mrengo wa Rais wa Zamani Joseph Kabila, wataendelea kumdharau

Tshisekedi amesema, “Wamenipa tabu sana, wanasubiri nishindwe kutimiza kazi yangu. Wananisukuma kufanya mambo ambayo sijapanga kufanya, kama ni kuvunja Bunge naweza kulivunja, na kama itabidi nifikie hatua hiyo sitachelewa kufanya hivyo,”

Katika hatua nyingine, Tshisekedi ametupilia mbali Madai ya kuwepo mpango wa kuigawa nchi hiyo akisema mazungumzo hayo hayana Msingi na ni mbinu za kutaka kuchelewesha Ajenda ya Maendeleo kwa Taifa hilo.

Rais Tshisekedi ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, aliingia katika maelewano na Chama cha Rais wa Zamani Kabila cha PPRD, kushirikiana naye katika Serikali yake, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018

DSTV yaja na ofa, kwa 29,000 tu, unaweza kutazama ligi zote Uingereza
Korogwe: Watu wasiojulikana waweka jiwe kwenye barabara ya treni