Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi amesema kuwa atawaachia huru wafungwa wote wa kisiasa ndani ya kipindi cha siku kumi kuanzia jana.

Akizungumza jana katika hotuba yake, Tshisekedi alisema kuwa amemuagiza Waziri wa Sheria kuhakikisha wafungwa wote walioko magerezani kwa sababu ya mitazamo yao ya kisiasa waachiwe huru.

Kupitia hotuba hiyo, Tshisekedi alizindua rasmi programu yake ya siku 100 za dharura kwa lengo la kuhakikisha kuna hali ya utulivu wa kisiasa nchini humo.

“Katika kukazia ukuaji wa kidemokrasia nchini kwetu, nimeupa kipaumbele mpango wa kupunguza taharuki,” BBC wanamkariri.

“Nimemuagiza waziri wa sheria kufanya kila liwezekanalo kisheria kuwaachia huru watu wote wanaoshikiliwa magerezani kwa makosa yanayendana na kutoa maoni yao kisiasa, hususan katika kipindi cha maandamano yaliyofanyika kabla ya uchaguzi,” alisema Rais wa DRC.

Katika hotuba yake pia alitoa mwanga wa kuwaruhusu kurejea nyumbani, watu waliokimbilia uhamishoni kutokana na sababu za kisiasa.

Polisi watawanya waandamanaji walioziba njia ya kwa Waziri Mkuu
Lema ‘atoa povu’ kuhusu Lowassa, Nassari akiri kuhuzunika