Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja kufuatia nwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoia Dkt. John Magufuli.

Zwede amepokelewa na Mwenyeji wake Rais Magufuli kwenye Uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita saa nne asubuhi ya leo ambapo kabla ya kuendelea na ziara anatarajiwa kuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Magufuli.

Sahle ni Rais wa kwanza Mwanamke Ethiopia na Mwanadiplomasia mwenye uzoefu na amewahi kuwa Balozi wa Ethiopia Nchini Senegal na Djibouti.

Kabla ya kuwa Rais wa Ethiopia, Sahle-Work alikuwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika.

Ilanfya, Matheo kuanza mazoezi KMC FC
Mputu, Ulimwengu kuiongoza TP Mazembe Simba Super Cup