Rais wa klabu bingwa nchini Hispania, FC Barcelona, Joseph Maria Bartomeu amepinga vikali tetesi zinazopata nguvu kila kukicha akisema kamwe klabu hiyo haiwezi kumuuza mshambuliaji wao, Lionel Messi.

Rais huyo alisema wao wana mkataba na mchezaji huyo na ataendelea kuitumikia hadi pale atakapomaliza na wakiona kama kuna haja ya kumuongeza, watakaa chini na nyota huyo.

“Nimesikia tetesi za Inter Milan na Manchester City, mimi kama kiongozi mkuu sijui zinatoka wapi, Messi ana mkataba na Barca na haondoki,” alisema.

Comments

comments