Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka Tanzania, vigogo wa juu katika Shirikisho la Soko la kimataifa, Fifa na lile la Afrika, CAF watakuwa nchini kwa mkutano maalumu kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya soka.

Rais wa Fifa, Gianni Infantino atashiriki katika mkutano huo maalumu uliopangwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanzia kesho kutwa.

Mkutano unaojulikana kwa Fifa Executive Football Summit utashirikisha nchi wanachama 19 za Fifa na kufanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) na Tanzania kuwakilishwa na Rais na katibu wake mkuu.

Tanzania ni nchi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati iliyopewa heshima ya kuandaa mkutano huo ambao pia utajadili masuala ya soka la wanawake, vijana na mfumo wa usajili wa kielektroniki wa TMS ambao kwa sasa utakuwa chini ya Fifa wenyewe na si wakala.

Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi mkubwa wa Fifa kutembelea Tanzania na kubwa zaidi ni kupewa    nafasi ya mkutano wa siku moja ambao utahudhuriwa na  viongozi wa mashirikisho ya soka katika nchi    mbalimbali.

Madhumuni hasa ya mkutano huo ni kuirejesha Fifa kwenye mpira na mpira wa miguu kwa Fifa, kupanga mikakati ya maendeleo ya siku za usoni ikiwa ni pamoja na mataifa 12 duniani kupewa heshima ya kuandaa mikutano hiyo.

”Hii ni heshima na tumepewa nafasi kutokana na utawala bora ambao kwa kipindi cha cha miezi mitano tangu tuingie madarakani tumeonyesha ” amesema Rais wa Shirikisho la soka Tanzania , TFF, Wallace Karia.

Mataifa yatakayoshiriki mkutano huo ni Bahrain, Palestina, Saudi Arabia, United Arabs Emirates (UAE), Algeria, Burundi, Afrika ya Kati, Ivory Coast, Mali, Marocco, Niger, Tunisia, Bermuda, Monserrat, St.Lucia, Us Virgin, Maldives, Congo brazzaville na Wenyeji Tanzania.

 

Video: Linah aja na ''Same boy'' kama ya R-Kelly na Usher ''same girl''
Halmashauri ya Jiji Dar kuingiza milioni 160 kutoka Uber