Rais wa Ghana Akufo-Addo ameamrisha kukamatwa mwenyekiti wa shirikisho la kandanda la Ghana Kwesi Nyantekyi, ambaye pia ni makamu wa rais wa kwanza wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF.

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya kuandikwa kwa makala moja ya uchunguzi ambayo inamhusisha Kwasi Nyantekyi na vitendo vya ufisadi.

Uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi wa habari maarufu, Anas Aremeyaw Anas uliwasilishwa kwa rais wa nchi hiyo ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Aidha, inadaiwa kuwa ripoti hiyo imefichua vitendo vya ufisadi miongoni mwa maafisa wengine wa shirikisho la kandanda nchini Ghana.

Hata hivyo, Kwesi Nyantenkyi amekuwa rais wa shirikisho la kandanda nchini Ghana tangu mwaka 2005 na hajatamka lolote kuhusu kujiuzulu.

 

TFDA yawasaka wanaotangaza dawa za kuongeza maumbile
Orodha ya wanaowania tuzo VPL 2017/18