Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-U amepiga marufuku sherehe za ndoa na shughuli za misiba/matanga katika wiki hii wakati akijiandaa na sherehe ya kusimikwa kama kiongozi mkuu wa nchi hiyo wiki ijayo.

Taarifa zilizoripotiwa na Sunday Times, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 33 anatarajiwa kusimikwa rasmi uongozi wake katika sherehe hizo pamoja na kutangaza rasmi nchi hiyo kama nchi yenye silaha za ‘nyuklia’.

Katazo hilo ni la muda hadi sherehe yake itakapomalizika. Ulinzi mkali umeimarishwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Pyongyang, kuhakikisha hakuna muingiliano wowote na tishio lolote la kiusalama.

Naibu Waziri wa Congo aliyedakwa ‘akijichua’ ofisini atimuliwa
Young Africans Waacha Zogo Toto Africans