Rais mpya wa Malawi Lazarus Chakwera amewajibu waliomkosoa baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri lenye Mawaziri 31 huku Mawaziri 6 kati yao wakiwa ni Ndugu wa Familia moja.

“nimefanya uteuzi kwa kuzingatia sifa kwenye kazi, sidhani kama uhusiano wao wa Kifamilia, kabila au Dini unatuathiri, Undugu hauna madhara kama wanajua majukumu yao” Amesema Rais huyo.

Wiki chache baada ya kuapishwa, Rais huyo alipata upinzani mkubwa baada ya ya raia wa Taifa hilo kuanza maandamano dhidi yake wakimkosoa kuteua watu ambao ni ndugu kwenye Baraza la Mawaziri.

Rais Chakwera anadaiwa kuteua baadhi ya Mawaziri akiwemo mume na mke na wengine ni kaka na dadaake huku 70% ya Baraza hilo ikidaiwa kuhusisha watu wa jamii moja na yeye.

Mwanaharakati wa masuala ya kijamii, Mkotama Katenge Kaunda alisema hatua hiyo inakera kwa kuwa Rais aliahidi kwamba Malawi mpya itakabiliana na upendeleo na ukiritimba.

Marufuku ya uuzaji wa pombe Afrika Kusini yarejea kukabili Corona
Magufuli ateua Bosi mpya TIC

Comments

comments