Rais wa Mauritius Ameenah Gurib-Fakim ametangaza kujiuzulu huku kashfa ya kifedha ikiwa inaendelea kumuandama.

Gurib-Fakim ambaye alikuwa rais pekee mwanamke Barani Afrika ameshutumiwa kwa kununua vitu binafsi vya kifahari vyenye thamani ya maelfu ya dola kwa kutumia kadi ya benki ya Taasisi ya Dunia yenye makao yake nchini Uingereza.

Gurib-Fakim alisema mapema wiki hii kwamba aliitumia kadi bila kujua, lakini alikuwa amewarudishia fedha hizo.

Hata hivyo, Rais huyo alichaguliwa kuwa  rais mwaka 2015 na hapo awali alikuwa Profesa wa kemia katika kitivo cha sayansi cha Chuo Kikuu cha Mauritius.

Mkapa akerwa matokeo mabaya shule za Serikali, ataka suluhisho
Ulega kuibadiri sekta ya Mifugo na Uvuvi