Hatimae uongozi wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris St Germain, umefikia maamuzi ya kuachana na meneja Laurent Blanc kwa kumuamuru aondoke klabuni hapo.

Usiku wa kumakia hii leo taarifa za kuondoka kwa Blanc zilitolewa kwenye tovuti ya gazeti la michezo L’Equipe.

Taarifa hizo zimeeleza kwamba, meneja huyo mwenye umri wa miaka 50, ameondoka klabuni hapo ikiwa ni baada ya miezi minne kupita ambapo ilishuhudiwa akisaini mkataba mpya wa miaka miwili.

Hata hivyo taarifa hizo zimeendelea kubainisha kwamba PSG, wamekubali kumlipa fidia ya Euro milioni 22 kwa kuvunja mkataba huo.

Blanc ameondoka PSG, kwa kukabiliwa na changamoto ya kushindwa kufanya vyema kwenye michuano ya barani Ulaya, ambayo imekua dhumuni kubwa kwa uongozi wa sasa, kutokana na uwekezaji uliofanywa.

Raisi wa PSG, Nasser al Khelaifi alimtaka Blanc kufanikisha mipango ya kukiwezesha kikosi chake kutwaa ubingwa wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2015-16, lakini mpango huo ulishinidikana kwenye hatua ya robo fainali baada ya kukubali kufungwa na Man city.

Upande wa michuano ya ndani ya nchini Ufaransa, Blanc alionekana kufaulu kwa kiasi kikubwa kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi daraja la kwanza (Ligue 1) mara tatu, Kombe la Ufaransa (French Cup) mara tatu,  Kombe la ligi (League Cup) mara tatu  pamoja na Ngao ya jamii (Trophée des Champions) mara tatu.

Mbunge CCM ataka Mbwa, Michango ya Misiba, Sadaka, harusi, kulipiwa kodi
Entente Setif Yaondolewa Ligi Ya Mabingwa Afrika