Rais wa Syria Bashar al –Asaad amefanya ziara ya ghafla nchini Urusi ambapo amekutana na rafiki yake rais Vladmir Putin aliyemsaidia katika kupambana na waasi bila kueleza wazi.

Ziara hiyo ya ghafla imeelezwa na msemaji wa Rais wa Urusi, Dmitry Peskov kuwa ni ziara ya kikazi iliyoanza Jumanne ya wiki hii ambapo alifanya mazungumzo na mwenyeji wake kuhusu vita dhidi ya magaidi wa Islamic States (IS) na makundi mengine nchini Syria.

Mwezi  uliopita, Urusi ilituma ndege zake nchini Syria na kufanya mashambulizi katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi lakini rais wa Urusi alisisitiza kuwa walilenga maeneo ya makundi ya magaidi.

Wakati rais Asaad akiwa Urusi, ndege za Marekani zimeendelea kufanya mashambulizi nchini Syria zikilenga maeneo yanayokaliwa na kundi la Islamic State huku wakiwapatia silaha nzito waasi kwa madai kuwa wanawasaidia kupambana na kundi la IS.

Hii inatajwa kuwa ziara ya kwanza kufanywa Rais Assad nje ya nchi tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria 2011.

Mvuto wa Sura na Umbo wachangia Kuwapa Ushindi Wapinzani, Licha Ya Tafiti Kutowapa Ushindi
Magufuli Ageukia Kura Za Ushindi Dar