Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu rambirambi kwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva kutokana na kifo cha shabiki wa timu hiyo, Shose Fedeline aliyefariki dunia jana mchana Mei 28, 2017 katika ajali ya gari.

“Nakuandikia Rais wa Simba, Evans Aveva, pia ndugu, jamaa na marafiki pamoja na majirani wa marehemu Shose Fideline na wanafamilia wengine wa mpira wa miguu, kwamba nimepokea taarifa za ajali ya gari iliyosababisha kifo cha mmoja wa mashabiki wa timu ya Simba kwa masikitiko makubwa sana. wito wangu, nawaomba wanafamilia wote kuwa watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Malinzi.

Hata hivyo, Msiba wa shabiki huyo wa Simba umetokea wakati Simba imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Azam, hivyo kuwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) hapo mwakani.

 

Picha 15: Mbio za Mwenge wa Uhuru Ilala, Dar es salaam
Video: Foby ajiweka kando ya Diamond na Ali Kiba, amvuta Lady Jay Dee

Comments

comments