Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Ndugu Wallace Karia amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani “Profesa Majimarefu” aliyefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili usiku wa kuamkia jana.

Rais wa TFF Ndugu Karia amesema Profesa Majimarefu alikuwa mwanamichezo kwa vitendo akishiriki katika mambo mbalimbali ya Mpira wa Miguu.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Profesa Majimarefu ambaye hakika alikuwa mwanamichezo wa kweli akishiriki kwa vitendo hata katika jimbo lake la Korogwe Vijijini,Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa Familia,ndugu,Jamaa na marafiki” alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.

Aidha Rais wa TFF Ndugu Karia amepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Polisi Dar Awadh Kilewa na kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa wafiwa,familia,ndugu,timu ya Polisi Dar na marafiki.

Amesema kifo cha Awadh kimeshtua hasa kutokana na kuwa bado mchango wake ulihitajika katika Mpira wa Miguu.

“Mchango wa Awadh kwenye Mpira wa Miguu bado ulikuwa ukihitajika katika Timu yake ya Polisi na mpira wa miguu kiujumla,Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi,Amina.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 5, 2018
Mtibwa Sugar kushiriki kombe la shirikisho kwa masharti

Comments

comments