Rais wa Tunisia, Beij Caid Essebsi amefariki dunia katika hospitali ya kijeshi iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.

Taarifa za kifo chake zimetolewa kupitia ukurasa wa facebook kwa lugha ya Kiarabu na kwamba amefariki asubuhi ya leo.

Rais Essebsi alipelekwa katika hospitali ya jeshi jana jioni kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.

Aidha, Essebsi mwenye umri wa miaka 92, amekuwa madarakani tangu mwishoni mwa mwaka 2014.

Hata hivyo, rais huyo alikuwa akijitokeza mara chache hadharani tangu wakati huo na alitia saini amri ya rais kuanzisha mchakato wa uchaguzi wa bunge na rais nchini humo uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Video: Tazama mzee Kilomoni alivyokamatwa na polisi leo akiongea na waandishi wa habari
JPM aagiza yafanyike marekebisho ya sheria ya TAZARA