Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amelipongeza jeshi la nchi hiyo kwa kufanikiwa kuzidisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya Urusi nchini humo.

Kupitia hotuba yake kwa njia ya video, Zelensky amesema katika muda wa wiki moja iliyopita, jeshi la Ukraine lilipata mafanikio makubwa katika kuharibu mikakati ya jeshi la Urusi.

Amesema kila shambulizi dhidi ya hifadhi ya risasi za Urusi, vituo vya kamandi yake na mkusanyiko wa vifaa vya Urusi linaokoa maisha ya wote na maisha ya wanajeshi na raia wa Ukraine.

Zelensky amezungumzia mafanikio madogo ambayo jeshi la nchi hiyo limeyapata kwenye majimbo ya Kherson na Zaporizhzhia yaliyokamatwa na Urusi miezi ya hivi karibuni.

Vikosi vya Ukraine vimemudu kuyakomboa baadhi ya maeneo ya majimbo hayo lakini sehemu kubwa ardhi ya mikoa hiyo bado inadhibitiwa na Urusi.

Katibu Mkuu atunukiwa uraia wa heshima Japan
Mfahamu mwanasiasa mkongwe nchini Kenya Raila Amolo Odinga