Saa chache baada ya kufanyika jaribio la kuipundua serikali ya Uturuki inayoongozwa na Rais Tayyip Erdogan, Rais huyo amesema kuwa mpango mzima wa kumpindua ulisukwa katika jiji la Pennsylvania nchini Marekani.

Akihutubia taifa hilo lililo katika hali ya taharuki kubwa, Rais Erdogan amesema kuwa waandaaji wa tukio hilo ni kundi la kidini la Cleric Fethullah Gulen ambalo kiongozi wake anaishi uhamishoni katika jiji la Pennsylvania nchini Marekani.

“Uturuki haiwezi kuogopeshwa na aina hii ya mapigano na Uturuki haiwezi kuongozwa kutoka Pennsylvania,” alisema Rais Erdogan mapema leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Istanbul.

“[Waliofanya jaribio hili] waliambiwa kufanya hivyo kutoka Pennsylvania,” aliongeza.

Gulen aliikimbia Uturuki mwaka 1999 baada ya kutuhumiwa na kusakamwa na Serikali akidaiwa kuendesha siasa zenye mlengo wa imani ya kali ya Kiislam.

Harakati baada ya jaribio la Mapinduzi kushindikana

Harakati baada ya jaribio la Mapinduzi kushindikana

Rais huyo alieleza kuwa nchi imerudi katika hali ya usalama kama kawaida na kwamba wote waliohusika watakumbwa na adhabu ya kosa la uhaini kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.

Wanajeshi na polisi walioshiriki kufanya jaribio la mapinduzi usiku wa kuamkia leo wamejisalimisha. Watu zaidi ya 90 wameuawa na wengine 1500 wamekamatwa.

Aliyeoongoza kidato cha 6 ni tunda la Shule ya Kata, aeleza alivyodharauliwa
Kichupa: Shilole, Lina Kwenye ‘Too much’ ya Darassa