Marekani imempiga marufuku Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh kuingia nchini humo kutokana na historia mbaya ya utawala wake iliyohusisha vitendo vya rushwa na uvunjifu wa haki za binadamu.

Uamuzi huo umetolewa jana ikiwa ni miaka miwili tangu Jammeh alipolazimishwa kukimbilia uhamishoni nchini Equatorial Guinea. Aliondolewa kwa nguvu madarakani na Jeshi la Umoja wa Afrika baada ya kukataa kuachia madaraka kufuatia kushindwa kwenye uchaguzi mkuu na Adama Barrow.

Yahya Jammeh na mkewe Zineb Yahya Jammeh

Marekani imeeleza kuwa Jammeh amezuiwa kuingia nchini humo pamoja na familia yake yote, na kwamba uamuzi huo unatokana na sheria za nchi hiyo kwa maafisa wa Serikali za nchi nyingine ambao wanaaminika kujihusisha na vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa Serikai ya Gambia inayoongozwa na Barrow, Jammeh aliiba zaidi ya $50 milioni za umma alipokuwa madarakani.

Kwa mujibu wa ripoti, Jammeh anamiliki majumba katika eneo la Potomac, Maryland nchini Marekani, Kilometa 24 tu kutoka Washington. Alinunua majumba hayo mwaka 2010 kwa $3.5 milioni kutoka kwa mwanamichezo wa Marekani, Calbert Cheaney.

Uwekezaji katika sekta ya madini waongezeka
Waziri kuitwa ‘Kahaba’, Afrika Kusini yaiwakia Rwanda