Mahakama nchini Senegal jana ilimhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa Rais wa Chad, Hissene Habre kwa makosa ya dhidi ya haki za binadamu.

Mahakama hiyo imemkuta na hatia Habre kwa makosa ya ubakaji, kuwashikilia watu mateka pamoja na mauaji ya zaidi ya watu 40,000 katika kipindi cha uongozi wake kati ya mwaka 1982 na 1990.

Hata hivyo, Habre ameupinga uamuzi huo na kukataa kutambua uhalali wa mahakama hiyo. Hakuonesha kushtushwa na uamuzi huo baada ya kusikia kauli ya mahakama.

Mwaka 2005, Mahakama ya Ubelgiji ilitoa hati ya kumkamata Habre ikieleza kuwa ina mamlaka ya jumla (universal jurisdiction) lakini Mahakama ya Senegal iliiwasilisha ombi lake kwa Umoja wa Afrika na kupewa ridhaa ya kuendesha kesi hiyo kwa niaba ya Umoja huo.

 

 

 

 

Joe Ledley Kucheza Euro 2016
Diego Simeone Apania Kumrejesha Diego Costa

Comments

comments