Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, ambaye pia aliwahi kuhudumu kama Rais wa nchi hiyo amefariki akiwa na umri wa miaka 93.

Peres ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi lakini madaktari wameeleza kuwa hali yake ilikuwa mbaya zaidi tangu wiki mbili zilizopita.

Kiongozi wa Palestina Yasser Arafat (kushoto), Waziri wa mambo ya zamani wa Israel wakati huo Shimon Peres (katikati) na Waziri Mkuu wa  Israel  Yitzhak Rabin wakionesha tuzo zao za amani za Nobel

Kiongozi wa Palestina Yasser Arafat (kushoto), Waziri wa mambo ya zamani wa Israel wakati huo Shimon Peres (katikati) na Waziri Mkuu wa Israel Yitzhak Rabin wakionesha tuzo zao za amani za Nobel

Kiongozi huyo  wa zamani wa Israel atakumbukwa kwa juhudi zake kubwa za kuleta amani mashariki ya kati ambapo mwaka 1994 alikabidhiwa tuzo ya amani ya Nobel akiwa waziri wa mambo ya nje, pamoja na viongozi wengine wa Palestina Yasser Arafat na Waziri Mkuu wa Israel wa wakati huo, Yitzhak Rabin.

Uamuzi wa kesi ya mauaji ya dada wa bilionea kusomwa okt 10
CUF wamfukuza rasmi Profesa Lipumba