Rais wa Zambia na kiongozi wa chama cha Patriotic Front (PF), Edgar Lungu ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, akipata ushindi mwembamba dhidi ya mpinzani wake, Hakainde Hichilema wa United Party for National Development (UPND).

Matokeo yaliyotangazwa jana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zambia yameonesha kuwa Lungu amepata ushindi wa asilimia 50.35 ya kura zote dhidi ya asilimia 47.67 ya Hichilema.

Hata hivyo, upande wa upinzani umepinga vikali matokeo hayo ukieleza kuwa kura zilichakachuliwa ili kumpa ushindi rais Lungu.

Mwanasheria wa UPND, Jack Mwiimbu aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanauhakika na wanaushahidi kuwa kura zilichakachuliwa na wamepanga kupinga matokeo hayo mahakamani.

“Tuna ushahidi kuwa kura za Hakainde Hichilema zilichakachuliwa na kupunguzwa na Tume ya uchakuzi,” alisema mwanasheria huyo.

Uchaguzi wa nchi hiyo ulishuhudiwa kuwa na upinzani mkali huku visa vya hujuma vikitupwa kwa kila pande.

 

Amissi Tambwe Arejesha Majibu Kwa Wanaotaka Ushindani
Antonio Conte Azima Minong'ono Ya Cesc Fabregas