Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 119 cha katiba ya Zanzibar amefanya uteuzi wa wajumbe 6 wa Tume ya uchaguzi Zanzibar.

Katika uteuzi huo Shein amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Mahmoud Hamid kuwa mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi wa Zanzibar.

Aidha amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Mabruki Jabu Makame, Fateh Saad Mgeni, Makame Juma Pandu, Dk. Kambo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdulla na Bi Jokha Khamis Makame.

Uteuzi huo umeanza rasmi leo Juni 20, 2018 ambapo wajumbe wote wa Tume ya uchaguzi waliotajwa wanatakiwa kufika Ikulu siku ya Ijumaa ya tarehe 22 juni 2018 saa 4 asubuhi tayari kwa kuapishwa.

Jaji Mutungi avitahadharisha vyama vya siasa
Wagonjwa 11 wafanyiwa upasuaji wa Moyo JKCI