Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe hawezi kutembea kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.

Kwa mujibu wa Rais Mnangagwa, Mugabe mwenye umri wa miaka 94 anaendelea kupatiwa matibabu nchini Singapole ambapo alimekaa kwa miezi miwili. Amesema Serikali yake itaendelea kumhudumia kwa kadiri iwezavyo kwani ndiye muasisi wa Taifa hilo.

“Hivi sasa ni mzee. Ni Dhahiri, hawezi kutembea lakini chochote anachotaka tutampatia. Tunamhudumia. Yeye ni muasisi na baba wa Taifa la Zimbabwe. Ni baba wa ukombozi na uhuru wa Zimbabwe,” Rais Mnangagwa aliiambia AFP.

Mugabe alikuwa Rais wa kwanza wa Zimbabwe, aliyeongoza na kufanikisha ukombozi dhidi mataifa ya kikoloni ya Ulaya. Ameiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 37, akianza kama Waziri Mkuu na mwaka jana alijiuzulu Urais kwa shinikizo la jeshi.

Rais Mnangagwa aliingia madarakani baada ya Mugabe kujiuzulu kwa shinikizo la jeshi na maandamano ya wananchi wasiomuunga mkono. Alishinda katika uchaguzi uliofanyika miezi michache baadaye.

Waziri mpya wa kilimo atangaza kiama, "Serikali imepokea malalamiko mengi kwa wananchi"
Boti yazama ziwa Victoria ikiwa na abiria 90 wakisherehekea

Comments

comments