Bunge limepiga kura kupitisha marekebisho ya Katiba na kuondoa ukomo wa rais kukaa madarakani ambapo Rais wa sasa Xi Jinping ameruhusiwa kutawala bila kikomo.

Katika mchakato huo ulihusisha Wabunge takribani 3000 waliopiga kura na wakati wa kutolewa kwa matokeo ni Wabunge wawili tu ndio walipiga kura ya hapana dhidi ya mabadiliko hayo

Aidha, Katiba ya China ilikuwa ikitoa uhalali kwa Rais kukaa madarakani kwa muda usiozidi vipindi viwili tu huku kila muhula ukiwa hauzidi miaka 5 (kama ilivyo kwa Katiba ya Tanzania)

Hata hivyo, Mwezi uliopita chama cha Kikomunisti cha China kinachoongoza taifa hilo kilitoa pendekezo la kuondolewa kwa ukomo wa mihula ya Rais na Makamu wa Rais na leo wamehitimisha kwa kupiga kura.

 

Video: Sura mpya ya Dogo Janja yaibua hisia mpya
Manny Pacquiao amtaja mpinzani wake pambano lijalo