Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia, Zlatko Dalic ametangaza mipango yake kuelekea mchezo wa mwishoni wa kundi D, ambao utamkutanisha dhidi ya Iceland.

Dalic ambaye alifanikisha harakati za ushindi mnono wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Argentina usiku wa kuamkia jana, amesema kuelekea katika mchezo huo, baadhi ya wachezaji wake (Rakitic, Rebic, Mandzukic na Vrsaljko) atawapumzisha kufuatia kazi kubwa waliyoifanya tangu walipoanza kampeni ya kuusaka ubingwa wa dunia mwaka huu.

Kocha huyo amesema pamoja na kutambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Iceland ambao kama watashinda utawafanya kuweka rekodi ya kutinga hatua ya 16 bora wakiwa na alama 9, bado anaamini kazi hiyo itakamilishwa na wachezaji wengine ambao hawajacheza tangu walipowasili nchini Urusi.

Kwa upande mwingine Dalic amesema baadhi ya wachezaji hao wanakabiliwa na kadi za njano walizozipata katika michezo iliyopita, hivyo anahofia huenda wakashindwa kucheza katika hatua ya 16 bora, endapo wataadhibiwa tena katika mchezo dhidi ya Iceland.

“Baadhi yao wana kadi za njano, ninahofia huenda wakakosa kucheza mchezo wa hatua ya 16 bora ambao utakua muhimu sana kwetu,” amesema Dalic.

“Wamekua na msaada mkubwa sana kikosini tangu tulipoanza kucheza fainali za mwaka huu, lakini ninaamini waliosalia watakamilisha azma tunayoihitaji ya kumaliza michezo ya makundi, huku tukiwa na alama 9 mkononi.”

Craoatia wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora bada ya kuifunga Nigeria mabao mawili kwa sifuri na baadae kuikandamiza Argentina mabao matatu kwa sifuri.

Lil Ommy aiwakilisha TZ uzinduzi wa tuzo kubwa Afrika Mashariki, afunguka
Habari kubwa katika magazeti ya leo Juni 23, 2018