Mwenyekiti wa klabu ya Southampton, Ralph Krueger ana matumaini ya kuendelea kufanya kazi na meneja wa kikosi cha klabu hiyo Ronald Koeman, ambaye anahusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuondoka.

Krueger ameelezea matumaini hayo kufuatia mkataba wa meneja huyo kutoka nchini Uholanzi kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao.

Amesema wamekua na mazungumzo na ushirikiano mzuri na Koeman, na wakati wote huwa anamuhakikishia kuipenda klabu ya Southampton, ambayo ameisadia kufikia lengo la kucheza michuano ya barani Ulaya tangu alipowasili.

Mwenyekiti wa klabu ya Southampton Ralph Krueger (kushoto) akiwa na meneja wa klabu hiyo Ronald Koeman.

“Mwaka Ujao? Nina uhakika wa hali ya juu tutaendelea kuwa na Koeman, katika mipango yetu ya kuifikisha Southampton tunapopataka,” Alisema Krueger

“Pamoja na Mazonge yanayozungumzwa, lakini sina shaka na mtu huyu ambaye amekua mwema kwa kila mmoja klabuni hapa, hivyo kama kukubali Koeman ataondoka mwakani mimi nitakua mtu wa mwisho kuamini suala hilo.”

Koeman amekua akihushwa na mipango ya kutaka kupewa ajira ya kukinoa kikosi cha FC Barcelona ambacho kwa sasa kipo mikononi mwa meneja Luis Enrique.

Lupita Nyong’o adai hana TV nyumbani kwake, awataja wanaompa habari
Dar, Pwani, Morogoro zakabiliwa na tishio la nvua kubwa tarehe hizi