Shirikisho La Soka nchini TFF limetangaza orodha ya waamuzi watakaochezesha mchezo wanne wa Robo Fainali Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC), kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC.

TFF imemtangaza Ramadhan Kayoko wa Dar es salaam kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo huo utakaoanza mishale ya saa moja jioni Uwanja wa Taifa, akisaidiwa na Arnold bugado kutoka Tanga na Frank Komba wa Dar es salaam.

Orodha hiyo ya wamamuzi imetoka huku wadau wa soka nchini wakiendelea kulalamikia maamuzi yaliyoonyeshwa jana chini ya mwamuzi ya kati Shimari Lawi.

Lawi alichezesha mchezo wapili wa Robo Fainali Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC) kati ya Young Africans dhidi ya Kagera Sugar ulioamlizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Mwamuzi huyo analalamikiwa kwa kumuonyesha kadi ya nyekundu mchezaji wa Kagera Sugar Awesu Awesu pamoja na kutoa mkwaju wa penati kwa Young Africans, ambao unalalamikiwa haukuwa halali kutokana na Mrisho Ngassa kuangushwa nje ya eneo la hatari.

Hata hivyo waamuzi walipangwa katika mchezo wanne kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC wanatarajiwa kuwa makini wakati wote, ili kuepusha malalamiko yasiyo na lazima kutoka kwa wadau wa soka nchini kote.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na hisia kubwa hasa ukizingatia kwamba tayari watani wa jadi wa Simba SC, Young Africans wanamsubiri mshindi wa mchezo huo ili wakutane naye.

Kila timu inauhitaji mkubwa leo kushinda ili kukutana na Young Africans ambayo iliishinda Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa mabao mawili kwa moja.

Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba leo inahitaji kulipa kisasi cha kufungwa mechi mbili zote za Ligi Kuu Tanzania Bara walipokutana na Simba SC, huku Wanamsimbazi wakihitaji heshima pekee.

Fahamu maajabu ya Liverpool, Gundu la Klopp na Mane kwenda Madrid (Video)
Chifu alia na mtendaji aliyekata mti wa kimila "rudisha mizimu yangu"