Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa amesema kuwa Ujerumani ni mshirika muhimu wa kiuchumi wa nchi hiyo ambapo ameonyesha matumaini  juu ya ushirikiano huo kupanua fursa za uwekezaji wa Ujerumani katika nchi yake.

Ramaphosa ameyasema hayo jijini Cape Town wakati rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier akimaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.

Ramaphosa amesema kuwa Ujerumani ni mshirika mkubwa wa tatu duniani wa kibiashara wa Afrika Kusini na ni  mmoja kati ya wawekezaji wakubwa wa kigeni katika nchi hiyo. amesema kuwa zaidi ya makampuni 600  ya Ujerumani yanafanyakazi nchini Afrika Kusini, ambapo yameweza kutengeneza nafasi zaidi ya laki moja za kazi.

“Kama ilivyoonekana katika mazungumzo yetu na viongozi wa makampuni ya Ujerumani mjini Berlin mwezi uliopita, Afrika Kusini inaonekana kuwa sehemu muhimu ya uwekezaji, na kuna hamasa kubwa kwa makampuni  ya  Ujerumani kupanua uwapo wao hapa.”amesema Ramaphosa

Hata hivyo, Ujerumani na Afrika Kusini zitakuwa wanachama ambao si wa kudumu katika baraza la Usalama la  Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2019 na 2020 na rais, Cyril Ramaphosa amesema wamekubaliana kwamba nchi zao  zitafanyakazi kwa pamoja kuhimiza amani ya dunia nausalama pamoja na kuimarisha mfumo wa ushirikiano wa  pamoja.

Amuua mpenzi wake na kumfanya kitoweo
Dereva wa lori adaiwa kuiba pipa 156 na kutoroka