Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaelekea Marekani, ambako wasaidizi wake wanasema anatarajiwa kushinikiza uwepo wa mazungumzo zaidi kati ya Urusi na Ukraine wakati wa mkutane wake na na Rais wa Marekani Joe Biden hii leo Septemba 16, 2022.

Ramaphosa ni miongoni mwa viongozi wa Afrika ambao wamedumisha msimamo wa kutoegemea upande wowote katika vita hivyo, huku Afrika Kusini ikijiepusha na kura ya Umoja wa Mataifa inayolaani vitendo vya Urusi na kutaka kusuluhishwa kwa upatanishi.

Waziri wa uhusiano wa kimataifa wa Afrika Kusini, Naledi Pandor amesema Ramaphosa atasisitiza haja ya mazungumzo wakati wa mikutano na Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris, ili kupata mwelekeo wa nchi itakaposhiriki Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juma lijalo.

Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa (Kulia) Picha na The Africa Report.com

Amesema, “Tungetaka mchakato wa diplomasia uanzishwe kati ya pande hizo mbili na tunaamini Umoja wa Mataifa lazima uongoze, maana tuliashiria kuwa tulifurahi kwamba mazungumzo ya usafirishaji wa nafaka yaliendelea vizuri na nafaka imeanza kusafirishwa.”

Pandor ameongeza kuwa, “Lakini katika muktadha wa Baraza Kuu, tutasisitiza kwamba kunahitajika juhudi kubwa zaidi katika kutafuta suluhu juu ya mzozo huu mbaya na kwamba njia pekee ya kufanya hivyo itakuwa kwa suluhu la mazungumzo.”

Rais Ramaphosa, pia anatarajiwa kusafiri hadi U.K. kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II siku ya Jumatatu ambapo tayari mialiko kwa Viongozi wa kimataifa wapataoo 500 imetolewa ili waweze kushiriki siku ya kumpumzisha kiongozi huyo aliyetawala uingereza kwa miaka 70.

Bungeni: Wenye malimbikizo ya madeni 'walegezewa kamba'
Wasiovuta Sigara hatarini kuugua Saratani ya Mapafu