Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri, ambapo Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo.

Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma, pindi palipotokea anguka la thamani ya Rand alilazimika kumfukuza na nafasi yake kuchukuliwa na Des van Rooyen

Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala ya biashara.

Aliyekuwa mke wake Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma, ameteuliwa kuwa waziri wa ofisi ya rais.

Rais, Ramaphosa, ambaye ni mfanya biashara wa umri wa miaka 65, katika hotuba yake ya taifa awali mwezi huu, aliahidi kupambana na rushwa na kuboresha uchumi wa nchi hio.

Aliingia madarkani baada ya mtangulizi wake kuondoka katika hali tete, akikataa shinikizo kubwa ya yeye kujiuzulu.

Utawala wa miaka tisa ya Zuma ulikumbwa na misukosuko ya shutuma za ufisadi wakati nchi ilikuwa ikipambana na madeni ya ndani pamoja na viwango vya juu vya ukosaji ajira.

Neymar huenda akaikosa Real Madrid Machi 6
Wasafi TV, Redio zapata leseni… kuwashwa