Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na kufanya naye mazungumzo jijini Pretoria hii leo Machi 16, 2023.

Rais Samia aliwasili Jijini Pretoria nchini Afrika ya Kusini hapo jana Machi 15, 2023, kwa ajili ya ziara ya Kiserikali ya siku moja akiwa ameambatana na ujumbe wake na zifuatazo ni picha za baadhi ya matukio wakati wa ziara hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wakati wakielekea kwenye Viwanja vya mapokezi ya Viongozi vilivyopo katika Ofisi za Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini wakati wa ziara yake tarehe 16 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa katika viwanja vya Mapokezi ya Viongozi vilivyopo kwenye Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wakati akimuonesha Majengo mbalimbali ya Mji wa Pretoria katika Ziara yake ya Kiserikali nchini Afrika Kusini Machi 16, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mapokezi ya Viongozi vilivyopo kwenye Majengo ya (Union Buildings), Pretoria nchini Afrika Kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa kabla ya kuanza mazungumzo Pretoria nchini Afrika Kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa yaliyofanyika katika Ofisi za Majengo ya Muungano, Pretoria.

Fedha za Rais Samia zinatupa morali kubwa: Young Africans
Nimechoka kusubiri, nitagombea urais: Mtoto wa Rais Museveni