Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos amesema kuwa hatua ya Mohamed Salah kumshika mkono kwanza ndiyo iliyosababisha mchezaji huyo wa Liverpool kuumia wakati wa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Ramos amedai kwamba, Salah angeendelea kucheza mechi hiyo iwapo angedungwa sindano kipindi cha pili hivyo kusingekuwa na tatizo lolote.

“Niliwasiliana na Salah kupitia ujumbe, alikuwa vyema. Angeendelea kucheza iwapo angedungwa sindano kipindi cha pili. nimefanya hivyo mara kadha lakini wakati ni Ramos alifanya jambo kama hilo, linang’ang’aniwa zaidi,”amesema Ramos

Aidha, Salah alianguka na kuumia vibaya kwenye bega wakati wa kipindi cha kwanza cha fainali ya vilabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Real.

Hata hivyo, Wakili mmoja nchini Misri amewasilisha kesi ya kutaka Ramos alipe fidia ya £874m kwa madhara na hasara aliyowasababishia raia wa Misri kimwili na kiakili.

 

Majaliwa: Hatuwezi kutangaza ongezeko la mishahara hadharani
Arsenal yamuweka matatani Rais Kagame

Comments

comments