Imefahamika kuwa Beki kutoka nchini Hispania Sergio Ramos hana mpango wa kuachana na klabu ya Paris Saint-Germain, na kwa sasa amejikita kujiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu hiyo haraka iwezekanavyo, kwa mujibu wa wakala wake.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 35, aliumia kigimbi mwishoni mwa mwezi Julai na kumfanya kuwa benchi, huku akikosa baadhi ya michezo ya Ligi ya Ufaransa msimu huu 2021-21.

Msimu uliopita ‘2020/21’ akiwa na Real Madrid alianza katika michezo 15 ya Ligi ya Hispania ‘La Liga’ ikiwa michezo michache zaidi ukilinganisha na michezo 35 alizoanza msimu wa 2019/20.

Alicheza michezo mitano tu kwenye mashindano yote kwa klabu hiyo mwaka 2021, sawa na dakika 395 dimbani, huku mara ya mwisho kuichezea timu ya Taifa ya Hispania ni dhidi ya Kosovo, mwezi Machi mwaka huu.

Kuumia kwa Ramos kumefanya asipate nafasi ya kuichezea klabu yake mpya ya PSG, huku taarifa zikisema klabu hiyo inafikiria kusitisha mkataba wake.

Hata hivyo, miamba hao wa Ligue 1 ilitangaza Ijumaa kwamba, Ramos anajiandaa kuanza mazoezi ndani ya juma hili na wakala wake amebainisha wazi kwamba, hataondoka Parc des Princes.

Morrison ajibebesha jukumu Simba SC
CCM yafanya uteuzi wa makatibu wa mikoa na wilaya