Klabu ya Juventus ya Italia inajipanga kumuweka sokoni kiungo wake kutoka nchini Wales, Aaron Ramsey katika dirisha lijalo la usajili la majira ya baridi baada ya nyota huyo wa zamani wa Arsenal kupoteza namba katika kikosi cha kwanza cha wababe hao wa Turin.

Taarifa hiyo imezifungua macho timu za West Ham, Everton na Newcastle United ambazo zimeanza kuulizia uwezekano wa kuipata huduma ya kiungo huyo ambaye mkataba wake na Juventus utafikia kikomo mwaka 2023.

Ramsey mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akipambana kuingia katika kikosi cha kwanza cha Juventus ambayo imepanga kuachana naye katika dirisha lijalo kama mchezaji huru.

Rambo ni miongoni mwa wachezaji wanaopokea mshahara mkubwa katika Ligi Kuu ya Italia Serie A, jambo ambalo linazipa ugumu timu nyingi zinazohitaji huduma yake.

Kiungo huyo anajua kila kitu kuhusu Ligi Kuu ya England baada ya kucheza kwa miaka 11 akiwa katika kikosi cha Washika Bunduki Arsenal ambao walimuamini tangu akiwa kinda.

Nyota huyo alijiunga na The Gunners mwaka 2008 akitokea Cardiff City baada ya kukosa nafasi alitolewa kwa mkopo kwenda Nottingham Forest, baadae alirejea na kuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha profesa Arsene Wenger.

Katika miaka 11 aliyokaa Arsenal, nyota huyo ana rekodi ya kuvutia baada ya kucheza michezo 371, akifunga mabao 65 na kutoa pasi za mabao 65 katika mashindano yote aliyocheza.

Nyota huyo mwenye miaka 30, katika kipindi chote alichodumu Arsenal alifanikiwa kushinda mataji matatu ya FA pamoja na Ngao za Jamii mbili, lakini alitimka mitaa ya Colney mwaka 2019 na kujiunga na Kibibi Kizee cha Turin kama mchezaji huru.

Taifa Stars yatajwa, kucheza ugenini Oktoba 07
Joshua aomba kurudiana na Usyk