Mmiliki wa klabu ya Aston Villa Randy Lerner, amethibitisha kufanya biashara na mfanya biashara kutoka nchini China, kwa ajili ya kumuuzia klabu hiyo iliyoshuka daraja katika msimu wa 2015-16, uliofikia tamati mwishoni mwa juma lililopita.

Mmiliki huyo wa The Villians, amethibitisha taarifa hizo kwa kuwafahamisha mashabiki wa klabu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki ligi daraja la kwanza nchini England.

Lerner ambaye ni raia wa nchini Marekani, amekiri kufanya biashara na Dr Tony Jiantong Xia, anaye miliki kampuni ya Recon Group, ambayo sasa inaijumuisha klabu hiyo ya mjini Birmingham.

Mmiliki mpya wa klabu ya Aston Villa Dr Tony Jiantong Xia

Lengo kubwa na Lerner, kuiuza klabu ya Aston Villa ni kutaka kuona inapiga hatua kubwa ya kuondoka ilipo sasa, ambapo dhahir imeonekana huenda utawala wake haukua na tija ya kusaidia mipango iliyokua imewekwa.

Hata hivyo Tony Xia, ameonyesha dhamira ya kufanya mabadiliko makubwa klabuni hapo, na tayari inaelezwa kwamba wakati wowote kuanzia sasa huenda meneja mpya akatangazwa, ili kufanikisha harakati za maandalizi ya msimu jao.

Aliyekua mmiliki wa klabu ya Aston Villa Randy Lerner

Aliyekua meneja wa klabu za Former MK Dons, West Brom pamoja na Chelsea, Roberto Di Matteo anatajwa katika mpango wa kufanya kazi ya umeneja klabuni hapo chini ya utawala mpya.

Lakini hata hivyo huenda Di Matteo akapata upinzani wa kusaka ajira yake, kutokana na pendekezo lingine ambalo linamuhusisha aliyekua meneja wa klabu ya Leicester City, Nigel Pearson.

Aston Villa ilionyesha kupoteza muelekeo wa kupambana katika michezo ya ligi kuu msimu wa 2015-16, ikiwa chini ya meneja kutoka nchini Ufaransa Remi Garde, ambaye hata hivyo alitimuliwa miezi miwili kabla ya msimu kufikia kikomo.

Watatu Ama Wanne Kuongeza Nguvu Leicester City - 2016-17
Stand Utd Wajipanga Na Msimu Wa 2016-17, Watano Watemwa