Kiungo kutoka nchini Croatia, Niko Kranjcar amekamilisha harakati za kujiunga na klabu ya Rangers ambayo msimu ujao itashiriki ligi kuu ya soka nchini humo.

Kranjcar, amekanilisha hatua za kujiunga na klabu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka klabuni hapi hadi mwaka 2018.

Kabla ya kukamilisha utaratibu huo, kiungo huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za QPR, Portsmouth na Tottenham Hotspur zote za nchini England alifanyiwa vipimo vya afya na kuonekana amekidhi vigezo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Kranjcar alikuwa nchini Marekani katika ligi ya MLS akiitumikia klabu ya      New York Cosmos, ambayo alifanikiwa kuitumikia katika michezo saba na kufunga bao moja.

Hatua ya kujiunga na klabu ya Rangers, inamuwezesha Kranjcar mwenye umri wa miaka 31, kukutana na wachezaji aliowahi kucheza nao alipokua QPR, Joey Barton na Clint Hill.

Jamie Vardy Kuendelea Na Leicester City
Amdai Mke wake Aliyebadilishana wakati wa Fumanizi- Kenya