Ikiwa tayari ni wiki moja imetimia tangu rapa 50 Cent anyanyuke na kuiacha interview ya Complex  baada ya kuulizwa maswali mengi kumuhusu rapa mwenzake French Montana ambaye inasemekana kuwa wawili hao hawapo sawa.

Mkongwe huyo wa hiphop amefayiwa mahijianao Jana Jumapili na Power break fast club ya Power 105, nakuulizwa tena kuhusiana na ugomvi unaoendelea kuhusiana na rapa French Montana ambapo amedai hajui French Montana ana tatizo gani.

Hata hivyo  rapa 50 Cent amekanusha kuwa hakumpiga rapa huyo bali kuna mtu aliandika tu mtandaoni taarifa hizo na zikasambaa baada ya kuulizwa swali kuhusu uhuma hizo ambapo alisema sio za kweli.

Aidha rapa French Montana hajatoa neno lake lolote kuhusiana na sakata hilo.

 

Lukuvi atimiza agizo la Rais Magufuli akabidhi ekari 715 Kigamboni
Makonda amwambia Magufuli '' Mkapa alinipa nauli''

Comments

comments