Rapa nguli nchini Marekani, Rick Ross anatarajia kufanya onesho nchini Kenya, Aprili 20, 2018.

Taarifa za mkali huyo kutumbuiza nchini humo zimethibitishwa rasmi jana kwenye uzinduzi wa albam ya Diamond platnumz ‘A boy from Tandale’ aliyo kuwa akiizindua kwenye ukumbi wa Kenya National Thriater uliopo Nairobi Nchini Kenya.

Diamond ambaye ameshirikiana na Rozay kwenye wimbo wa Waka Waka alitumia usiku huo kuwafahamisha mashabiki wa muziki nchini Kenya, kuweka kumbukumbu kuwa nguli wa muziki wa rap kutoka nchini marekani Rick Ross atatembelea nchini humo kwa mara ya kwanza mwezi ujao na kufanya onesho kubwa kwenye viwanja vya Carnivore .

Aidha, Rozay, mapema mwezi huu alikimbizwa hospitali kutokana na ugonjwa ambao kisanyansi unajuliana kama pneumonia, ugonjwa huo unasababishwa na bakteria ambao hushambulia mapafu na kumsababishaa kushindwa kupumua vizuri.

Mourinho asisitiza De Gea kutokuondoka Old Trafford.
Wazazi wafariki dunia, mtoto anusurika