Rapper Swae Lee amepasuliwa mdomo baada ya kurushiwa simu na shabiki wa kike wakati akiwa jukwaani.

Shabiki huyo alimuomba Swae Lee apige nae picha kupitia simu yake, lakini mambo yalienda ndivyo sivyo na kuamua kuirusha na kupelekea kumjeruhi kwenye sehemu ya mdomo wake

Tukio hilo limetokea huko Dallas nchini Marekani wakati wa ziara inayowaunganisha Wiz Khalifa na kundi la Rae Sremmurd  ambapo  rapa huyo amepanga kumfungulia mashtaka shabike huyo.

Aidha, Picha za video zilizosambaa mtandaoni zinamuonesha  Lee  akimpiga mkwara shabiki huyo aliyerusha simu na kumjeruhi  huku msanii mwenzie wa kundi la Rae Sremmurd, Slim Jxmmi akajaribu kumtuliza bila mafanikio, huku msanii huyo akimtaka mtu wa Kamera kupiga picha ya karibu ili mashabiki walio hudhulia onesho hilo wawezo kuona jeraha alilolipta.

Gattuso achukizwa na Bakayoko
Bobi Wine na wenzake waachiwa huru kwa dhamana