Beki kutoka nchini Ufaransa Raphael Varane, ametajwa kuwa katika orodha ya wachezaji watakaosajiliwa na klabu ya Man Utd, endapo uongozi wa klabu hiyo utaridhia kumpa majukumu ya umeneja Jose Mourinho.

Varene ambaye aliwahi kufanya kazi na Jose Mourinho wakati akiwa na klabu ya Real Madrid, ametajwa kuwepo kwenye orodha ya meneja huyo kutokana na uwezo wake ambao umekua ukimkosha mkufunzi huyo kutoka nchini Ureno.

Gazeti la AS linalochapwa nchini Hispania, limedokeza kuwa usajili wa kwanza kwa Mreno huo endapo atakwenda Old Trafford, utamuhusisha  beki huyo wa Real Madrid.

Gazeti hilo limedai kuwa Mourinho aliyetupiwa virago huko Stamford Bridge mwishoni mwa mwaka jana, ni shabiki mkubwa wa Varane, aliyemsajili mwaka 2011 akitokea nchini kwao katika klabu ya Lens.

Akimzungumzia Varane mwaka juzi, Mourinho alisema: “Nafikiri ni beki wa kati kinda aliye bora zaidi duniani… Mchezaji kijana ni lazima awe mtu ambaye anacheza kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia, hawa ni wachezaji kama Hazard, Neymar na Rafa Varane. Labda nimesahau wengine.”

Jamal Malinzi Ampongeza rais Mpya wa FKF
Liverpool Yaingia Katika Vita Ya Kumuwania Chicharito