Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mtibwa Sugar ya Morogoro wamemsajili mshambuliaji wa Mwadui FC ya Shinyanga, Rashid Mandawa.

Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema kwamba mbali na mshambuliaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, pia wamemsajili beki wa kati Cassian Ponera kutoka Ndanda FC ya Mtwara.

Bayser pia amesema wamefanikiwa kuwaongezea mikataba wachezaji wao kadhaa wakiwemo kipa Said Mohamed na beki wa kati Salim Mbonde.

“Usajili unaendelea kwa umakini mkubwa chini ya Mwalimu Salum Mayanga kuziba mapengo hususan kwenye eneo la kiungo ambako tumeondokewa na Mzamiru Yassin, Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya ambao wote wameenda Simba,”amesema Bayser.

Mabigwa hao wa 1999 na 2000 wa Ligi Kuu, wanatarajiwa kuanza rasmi mazoezi Jumatatu hii kujiandaa na msimu mpya.

Bayser amesema kambi ya mazoezi itaanzia Dar es Salaam kabla kuhamia makao makuu ya timu, Manungu, Turiani mkoani Morogoro wiki moja baadaye.

Gwajima anasa mikononi mwa polisi, simu zake zapekuliwa
Polisi wasusa kulinda baada ya wachezaji kuvaa fulana kuhusu Weusi waliouawa