Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Ceser Manzoki amewaaga rasmi viongozi, wachezaji na mashabiki wa klabu bingwa nchini Uganda Vipers SC.

Manzoki amecheza kwa mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo kwa miaka miwili na kuisaidia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uganda msimu wa 2021/22, huku akiibuka kinara wa ufungaji bora.

Mshambiliaji huyo mzaliwa wa DR Congo, ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wa kuaga, huku akiwashukuru wale wote wanaohusika na Vipres SC kwa mazuri waliomfanyia.

“Asante kwa upendo wako, sitasahau.” ameandika Manzoki

Hata hivyo Uongozi wa Vipers ulihitaji kumsainisha mkataba mpya siku chache baada ya Ligi Kuu ya Uganda kufikia kikomo kwa msimu wa 2021/22, lakini alikataa kwa kushinikiza hitaji la Changamoto mpya ya soka lake.

Manzoki aliyetwaa Tuzo tano katika Ligi Kuu ya Uganda msimu wa 2021/22, anahusishwa na mpango wa kujiunga na miamba ya soka nchini, klabu ya Simba SC, inadaiwa tayari ameshafikia makubaliano binafsi na uongozi wa klabu hiyo.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 28, 2022  
CHADEMA 'yawakalia kooni' Mdee na wenzake