Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula amemkabidhi Rais Mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete, tuzo aliyoipokea kwa niaba yake wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika Mei 17-21, 2022 Kisumu, Kenya.

Tuzo aliyokabidhiwa Dkt. Kikwete ni ya heshima na iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa), kwa kutambua juhudi zake za kuimarisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government).

kiipokea tuzo hiyo Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete alimshukuru Waziri Dkt. Mabula kwa kuonesha uaminifu wa kuitunza tuzo hiyo tangu alipokabidhiwa Mei mwaka huu hadi alimpomkabidhi.

Mtayarishaji wa mabango akitundika tangazo linaloonesha tarehe ya mkutano wa wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika Kisumu nchini Kenya

Wakati wa mkutano huo wa majiji, maarufu kama Africities uliobeba kauli mbiu ya mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063, mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo hali ya miundo mbinu kwenye miji na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa miji hiyo.

Mameya wa miji mbalimbali, Mawaziri wa serikali za mitaa walihudhuria mkutano huo kwa lengo la kutafuta suluhu ya changamoto zinazowasumbua wakazi wa miji yao, kama vile mipangilio mibaya ya majengo, mitaa pamoja na changamoto za  upatikanaji wa umeme.

RC aagizwa kuwashughulikiwa wafugaji wakorofi

Baadhi ya washiriki kutoka Mataifa mbalimbali wakiwa wameshikilia tuzo walizokabidhiwa wakati wa kilele cha Mkutano wa Viongozi wa Majiji uliofanyika Mei 21, 2022 Kisumu, nchini Kenya.
Saba wafariki katika ajali Dodoma
UN yalaani uvamizi majengo ya Bunge