Leo hiii Mei 28, 2018, katika viwanja vya Karemjee Dar kumefanyika ibada fupi ya kuuaga mwili wa marehemu Kasuku Bilago aliyekuwa Mbunge wa Buyungu na Naibu Waziri Kivuli katika wizara ya Elimu na Mafunzo.

Taarifa iliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imesema Mei 29, 2018 siku ya Jumanne asubuhi mwili utasafirishwa katika viunga vya jiji la Dodoma katika viwanja vya Bunge Dodoma na kuagwa na wabunge kisha kusafirishwa kwa ndege kuelekea Kibondo.

Mei 30, 2018 siku ya jumatano wananchi wa Jimbo la Buyungu watapata fursa ya kuuaga mwili katika eneo litakalotangazwa baadae.

Na alhamisi ya Mei 31, 2018 itakuwa siku ya mazishi rasmi ambayo yatafanyika Nyumbani kwa Marehemu huko Wilayani Kakonko, Kigoma.

Aidha Chadema imetoa wito kwa Wanachama, wapenzi na Watanzania wote tuendelee kuikumbuka familia ya Marehemu katika Sala na Dua katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mpendwa wao ili Mungu aendelee kuwapa faraja.

Maafisa wa Marekani watua Korea Kaskazini, wateta ya Trump-Kim
Video: Raia wa Mali amuokoa mtoto kishujaa Ufaransa, Rais amtunuku

Comments

comments