Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ pamoja na Wadhamini Wakuu wa Michuano ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kampuni ya Azam Media, leo wamepanga Ratiba ya michuano hiyo hatua ya 32 Bora.

Shughuli za upangaji wa Ratiba ya hatua hiyo imefanywa kwa njia ya Droo katika Studio za Azam TV jijini Dar es salaam, ikiwahusisha wachezaji wa zamani Aeid Mziba ‘Tekelo’ na Maalim Saleh ‘Romario’, Baraka Kizuguto (Afisa wa TFF) pamoja na mtangazaji Hassan Ahmed.

Katika hatua hiyo Mabingwa watetezi Simba SC wamepangwa kukutana na Dar City, Mchezo ambao utapigwa Jijini Dar es salaam, huku Young Africans wakiangukia kwa Mbao FC ya jijini Mwanza.

Azam FC nao watakua nyumbani Azam Complex, Chamazi wakipapatuana na Transit Camp. Namungo FC nao wamepata nafasi ya kucheza mchezo wa hatua hiyo wakiwa nyumbani Mkoani Lindi ambapo wataikaribisha Lindi City.

Ratiba ya Michezo mingine hatua ya 32 Bora ya ASFC.

POLISI TZ Vs NDANDA FC
BIASHARA UTD Vs MBEYA KWANZA
AFRICAN LYON Vs KAGERA SUGAR
KMC Vs RUVU SHOOTING
GEITA GOLD Vs TUNDURU KOROSHO
BIASHARA UTD Vs MBEYA KWANZA
AFRICAN LYON Vs KAGERA SUGAR
PAMBA FC Vs STAND FC
BAGA FRIENDS Vs CATAMINE FC
TANZANIA PRISONS VS RHINO RANGERS
COASTAL UNON Vs TO BOYS
MBUNI FC Vs LIPULI

Kibu Denis: Sitashangilia nikifunga
Picha ya Nyani aliyechunwa ngozi yamponza Kanye West