Kutokana na wingi wa watu waliojitokeza Uwanja wa Jamhuri kumuaga Hayati Dkt. John Magufuli, ratiba imebadilishwa ambapo imeelezwa mwili utaagwa na watu wachache uwanjani.

Imeelezwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa Wananchi kuaga kwenye mitaa ili watu wote waweze kutoa heshima zao za mwisho.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amesema baada ya watu wachache kuaga, mwili wa Dkt. Magufuli utatolewa Uwanjani na kupitishwa round about ya Jamhuri na kisha katika Barabara ya Iringa na kisha barabara ya Polisi.

Ametaja Barabara nyingine ambazo mwili utapitishwa kuwa ni Jamatini, Bunge, Morena, Emaus kuzungushia Barabara ya Waziri Mkuu hadi African Dreams na kutokea Barabara ya Arusha hadi Uwanja wa Ndege.

Trump asivyokubali kushindwa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 21, 2021