Chama cha soka nchini England FA, muda mchache uliopita kimekamilisha hatua ya upangaji wa ratiba ya hatua ya fainali ya michuano ya Emirates FA Cup.

Everton wamepangwa kukutana na mshindi wa mchezo wa Manchester United dhidi ya West Ham ambao unalazimika kurudiwa baada ya matokeo ya sare ya bao moja kwa moja yaliyopatikana mwishoni mwa juma lililopita kwenye uwanja wa Old Trafford.

Everton ambao wananolewa na meneja kutoka nchini Hispania, Roberto Martinez, walifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kuwachapa Chelsea mabao mawili kwa sifuri.

Watford, ambao waliushangaza ulimwengu baada ya kuwavua ubingwa Arsenal kwa kuwatandika mabao mawili kwa moja, wamepangiwa kucheza na Crystal Palace.

Kikosi cha Alan Pardew (Crystal Palace) kilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Reading, na kuwa sehemu ya timu ambazo zimeingia kwenye hatua nusu fainali.

Michezo ya hatua ya nusu fainali itachezwa kwenye uwanja wa Wembley Jijini London siku Jumamosi Aprili 23 na Jumapili Aprili 24.

Mchezo wa hatua ya fainali wa FA CUP utachezwa kwenye uwanja huo huo, Mei 21.

CUF wadai Serikali ni chanzo cha Maalim Seif kuishi Serena Hotel, wataja gharama ya chumba
Real Madrid Na Ndoto Za Kumsajili Eden Hazard Kwa Mtego