Klabu tano za ligi kuu ya soka nchini England, leo zitafanyiwa utaratibu wa kupangiwa michezo ya hatua ya nusu fainali ya chama cha soka nchini humo FA (Emirates FA Cup).

Timu hizo ni Manchester United, West Ham, Everton, Watford na Crystal Palace na Everton.

Watford, Everton na Crystal Palace tayari zimeshatinga kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao iliyopita, huku Man United na West Ham zikisubiri matokeo ya mchezo wa mkondo wa pili kufuatia sare ya bao moja kwa moja, yaliyopatikana kwenye uwanja wa Old Trafford, mwishoni mwa juma lililopita.

Michezo ya hatua ya nusu fainali itachezwa kwenye uwanja wa Wembley Jijini London siku Jumamosi Aprili 23 na Jumapili Aprili 24.

Mchezo wa hatua ya fainali wa FA CUP utachezwa pia uwanja wa Wembely hapo Mei 21.

Katika droo ya hii leo, timu zimepewa namba za vipira ambavyo vitawekwa kwenye Chungu, 1 – Crystal Palace, 2 – Everto ,3 – Watford, 4 – West Ham United na Manchester United.

Kinnah Phiri Ataja Sababu Za Kufungwa Na African Sports
Ligi Ya ZFA Pemba Kuanza Hii Leo