Kiuno Bila Mfupa wa enzi hizo, Ray C ameamua kufanya documentary maalum inayohusu jinsi alivyojiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na majanga yaliyomkuta baada ya kugeuka teja.

Mwimbaji huyo ambaye alifanikiwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya kwa msaada wa rais Jakaya Mrisho Kikwete na sasa anafanya kazi ya kuwasaidia watu waliothirika na matumizi ya ‘unga’, amewaambia mashabiki wake habari hiyo kupitia Instagram.

“Sitakiwi kuongea ila kwa sababu Documentary inakamilika muda si mrefu nimeona niwambie tu kuwa Ray C Foundation imepata Donor mkubwa sana kutoka Germany. Na tayari tumeshaanza kushoot Documentary ya maisha yangu ya Uteja!Documentary hii inanihisu Mimi kama mwanamuziki itaonyesha jinsi gani nilivyoanza kuvuta madawa ya kulevya na majanga yote niliyofanya ili niweze kununua unga na mengi sana mabaya niliyokutana nao kipindi niko hoi na unga!

Bondia Francis Cheka Kupanda Uliongo Wa Manchester
Mourinho Aipotezea Adhabu Ya John Terry