Msanii wa muziki nchini Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amesema bado anaimani na msanii wa filamu, Wema Sepetu na anaamini ipo siku msanii huyo atasimama tena.

Ray C ameandika waraka mrefu kwa Wema Sepetu akimpa nguvu katika kipindi hiki ambacho kila mtu amekuwa akimtupia mawe kutokana na kisambaa kwa video zake za ngono akiwa na aliyemtaja kuwa ni  “Future husband” wake.

Ray c amesema;

“Nakumbuka 2006 Mange alinipigia simu akaniambia anakuja nyumbani na mshiriki mmoja atakaeperform wimbo wangu kwenye kipengele cha Vipaji kwenye mashindano ya urembo ya (Miss Indian Ocean) na inabidi tumvalishe kama mimi nikamwambia sawa! walipofika nyumbani Kwangu nilimwangalia wema juu mpaka chini na alivyo mrefu, nikamwambia Mange huyu anashinda Miss Tanzania,nakumbuka alikuwa mwembamba, mrembo na mwenye aibu and I was like Wow!!!!.

Anyway kiufupi Nakupenda mpaka leo Wema, maisha ni kama milima! wewe bado ni mdogo sana na una nafasi ya kuwa utakacho! pamoja na yanayoendelea sasa bado moyo wangu una imani na wewe kuwa utasimama tena zaidi ya juzi jana na leo na Utakua. Never give up!

Dunia inaweza kukubadilikia kutoka kuwa kipenzi cha watu na kuwa Public enemy number one!Its normal!!!Its ok!ila kumbuka Familia yako ndio kila kitu!Please usihuzunike ukajiona wewe ndo mkosaji dunia nzima maana kila binadamu ana majanga yake ni Mungu tu ndio mkamilifu ingawa sio sababu ya kutufanya kurudia makosa over and over again!

Nakupenda na nina imani na wewe! Nakutakia kila la kheri katika maisha yako na natamani kumuona Wema Mpya.Lots of  love @wemasepetu ”. Rehema Chalamila.

Marekani yapeleka Wanajeshi 5,200 mipakani kuzuia wahamiaji
Dele Alli kubaki Spurs hadi 2024

Comments

comments